Wawakilishi wa watumiaji wa program za wazi chanzo wa
Hispania, wamefungua kesi dhidi Kampuni
kubwa ya mambo ya kompyuta ya Microsoft katika mahakama ya Umoja wa nchi za
Ulaya siku chache baada ya Kampuni hiyo kutozwa faini ya dola milioni 729, kwa
kushindwa kuwapa wateja wake uchaguzi wa brouza wanazotaka kutumia.
Wawakilishi hao Hispalinux wamesema kuwa Microsoft
wanawabania washindwe kuweka program za Linux kwenye kompyuta zilizowekwa
Windows wakati zinauzwa, hali inayowapa shida na usumbufu sana katika matumizi
ya kompyuta.
Mwanasheria na kiongozi wa Hispalinux Bwana Jose Maria Lancho amesema kuwa amefungua
mashtaka katika tawi la mahakama hiyo la
Madrid.
