Ripoti ya hali ya uchumi duniani imeonesha kuwa idadi ya watu wanaoishi
katika umaskini uliopindukia imeongezeka zaidi, huku jirani zetu wa
Kenya na Uganda wakiwa wamepiga hatua zaidi katika kupunguza idadi ya
watu wanaoishi katika umaskini wa kipato.
Kwa mujibu wa Ripoti ya World Bank iliyoripotiwa kwenye mtandao na
Global Monitoring Report 2013, Watu wanaoishi katika umaskini wa
kupindukia (wa kipato) ni 38.01% kwa Uganda, 43.37% kwa Kenya na
Tanzania ni 67.87%.
Hata hivyo, kwa kuwa tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hivi
karibuni Rwanda na Burundi wamejiunga nasi kwenye Jumuiya hiyo, tunaweza
kujifariji kuwa sisi si wa mwisho Afrika Mashariki, kwani tunaizidi
Burundi ambayo 81.32% wanaishi kwenye umaskini uliokithiri (wa kipato).
Nchi nyingine ndogo, isiyo na bandari na iliyotoka kwenye matatizo ya
mauaji ya kimbari na vita, Rwanda, ina asilimia ndogo zaidi ya maskini
kulinganisha na Tanzania, ambapo 63.17% ya Wanyarwanda wanaishi katika
hali ya umaskini. |