Ndugu zangu, nawakaribisha katika blogu hii mpya ninayoianza leo. Blogu hii itakuwa na habari za kiteknolojia za hapa nyumbani Tanzania na sehemu zingine za dunia zitakazokuwa katika lugha ya Kiswahili ili kutuweka Waswahili katika hali ya kujua kinachoendelea duniani humu.
Nakaribisha michango ya kuwaelimisha wadau wengine, maoni ya kunirekebisha na kunifundisha, mawazo mapya ya kujenga na hata masihala yasiyochafua hali ya hewa ili kuifanya blogu hii iwe hai.
KARIBUNI SANA.