![]() | ||||||
| Rob Summers akifanya mazoezi ya kutembea kutumia vifaa maalumu Amar Toor ameripoti maajabu mapya katika mtandao wa Engadget ambapo kijana mwenye umri wa miaka 26 aliyepooza mwaka 2006 baada ya kugongwa na gari ameweza kusimama mwenyewe baada ya kuwekea vipandikizi na wanasayansi wa vyuo vya University of Louisville, UCLA and Cal Tech. Kijana huyo mkazi wa Oregon, Rob Summers alipooza kutoka kifuani kwenda chini alipewa aina mbalimbali za matibabu bila mafanikio kwa miaka mitano, wiki hii madaktari walitangaza kuwa ameweza kusimama mwenyewe, na anaweza kutembea kwa msaada wa vifaa maalumu baaada ya kuwekewa vipandikizi vinavyotoa mawimbiumeme yaliyopangiwa kubadili mawasiliano yaliyokatwa yaliyokuwa yakimuwezesha kuutumia mwili wake. |
