Unajua kuwa Ipad pamoja na kutumika sana kwa burudani na mawasiliano, ni kifaa muhimu sana cha kielimu? Mtandao wa wikipedia unataarifu kuwa Ipad wakati ikitoka kwa mara ya kwanza, zaidi asilimia 80 ya vitabu vilivyowekwa humovilikuwa ni vya elimu kwa watoto. Pia inaripoti kuwa Ipad ni kifaa kinachotumika sana kwa watoto wanaosomea nyumbani ambapo vyuo vikuu vingi huko Marekani hukodisha kwa wanafunzi wake ili watumie kama visaidizi vya masomo. Wakati huohuo Ipad zimesaidi watoto wenye ugonjwa wa autism kujifunza kuwasiliana na kujichanganya kwenye jamii kwa urahisi sana.
|