Wapenzi wa muvu wakae mkao wa kucheki muvu za Warner Bros kupitia facebook. Hayo yameelezwa na Thomas Gewecke ambaye ni mkurugenzi wa ugavi wa Warner Bros kampuni kubwa la muvu na burudani, na kuripotiwa na Anam Alpenia wa mtandao wa redherring.
Muvu hizo ambazo kwa kuanzia imewekwa iitwayo Dark Knight, zitakuwa zikikodishwa kwa malipo na waangaliaji wataweza kutoa maoni yao juu ya muvu hizo zitakazokuwa katika ukurasa maalumu katika facebook.
Uamuzi wa kuweka muvu katika facebook umekuja kutokana na kuwa facebook hutembelewa na mamilioni ya watu kila siku, ambapo wachache tu wakikodi muvu hizo malipo yake yatakuwa makubwa kuliko teknoloji ya kununua na kuazima DVD.
Bongo movie mmeinyaka hiyo?

