Vijiji na vitongoji vilivyokuwa havina huduma za broadband nchini Uingereza, vitapata huduma hizo kwa teknolojia ya juu sana ambayo bado ipo kwenye majaribio.
Teknolojia hiyo ya LTE advanced ambayo ipo majaribioni, inatarajiwa kufanyiwa majaribio huko Cornwall UK kuanzia September 1 hadi mwishoni mwa December mwaka huu.
Teknolojia hiyo ambayo ni mwendelezo wa teknolojia ya 4G itakuwa na kasi ya kufikia 40 Mbps ambapo wastani wake utakuwa ni kasi ya 10 Mbps.
Watu wa kujitolea, ambao ni wakazi wa Newquay wanahitajika kushiriki majaribio hayo.
