Tuesday, May 31, 2011

ALL-IN ONE PC


PC mpya ya v300 (all–in-one systems) inayotengenezwa na kampuni ya LG inatarajiwa kuwa moto wa kuotea mbali kimauzo kutokana na utamu utakaokuwamo ndani yake ingawa ni ya gharama sana.
PC hiyo ambayo imejumlisha karibu kila kitu, katika kifaa chenye ukubwa wa monita ya LCD itakuwa na uwezo mkubwa kiufanisi na pia itakuwa inachukua nafasi ndogo kwenye desk inajumuisha mambo yafuatayo:
1.      screen ya inchi 23 ya touch screen na manjonjo ya 3D.
2.       Mewani za kuangalizia manjonjo ya 3D.
3.      Prosesa ya intel core i3, i5 au i7, kadi ya graphics ya Radeon HD 6650M.
4.      Memory ya GB 8 ya DDR 3 na Hard disk ya GB 750 au pungufu.
5.      DVD au Blue-ray pamoja na Bluetooth na vikorokocho mbalimbali vyo kiburudani na kikompyuta.
Mambo yote hayo yamo katika kasha moja tu lenye ukubwa wa monita ya LCD.
Kaa mkao wa kufaidi.