Sunday, June 5, 2011

Intaneti Imesababisha Ponografia Kuwa Juu


Ujio wa intaneti umesababisha ponografia kupanda juu kupendwa na kibiashara kwa kiwango cha kutisha. Hayo yametanabaishwa na mtandao wa topten review. 

Ukitanabaisha zaidi mtandao huo ulieleza kuwa kila sekunde moja dola za Marekani elfu tatu na ushee hutumika kununua huduma za ponografia, kila sekunde moja watumiaji 28,258 wa intaneti hutembelea tovuti ya ponografia, na kila dakika 39 video mpya ya ponografia hutengenezwa Marekani.

Mtandao huo unasema kuwa mwaka 2006 Wamarekani walivuna dola 2.84 bilioni kwa mauzo ya ponografia kupitia intaneti.

Pia imeelezwa kuwa kuna tovuti 4.2 milioni za ponografia ( asilimia 12 ya tovuti zote duniani ), asilimia 35 ya download zote duniani ni za ponografia (1.5 bilioni downloads).

Na watu asilimia 89 ya wanaowasiliana mtandaoni hutongozana ambapo mtu mmoja kati ya watu saba wanaotembelea intaneti ameshawahi kutongozwa.