Friday, June 24, 2011

Watafiti chini ya bahari kunufaika

Mtafiti akiandaa maiki kwa majaribio

Wakiwa wamevutiwa na ufanyaji kazi wa sikio la nyangumi anayejulikana kama orca au killer whale, wanasayansi wa Chuo kikuu cha  Stanford, wametengeneza microphone itakayokuwa uwezo wa kunasa sauti chini ya bahari kwa ufadhili wa Litton Systems Inc kampuni inayomilikiwa na kampuni ya Kimarekani inayotengeneza vifaa vya vita na ulinzi ya Northrop Grumman Corporation inayoongozwa na Wesley G. Bush.
Maiki hiyo itakayokuwa na uwezo wa kufanya kazi kwenye kina kirefu sana bila kuharibika kutokana na mkandamizo wa maji inaubora kuliko maiki za aina hiyo zinazouzwa sasa
Orca wana uwezo mkubwa sana wa kusikia na wanasayansi hao wamenakili sikio la nyangumi huyo kupata kifaa hicho.