Ikiwa ni siku chache tu toka msimu wa mvua uliposita shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kupitia press release namba MPR/PR/12 23/06/2011 kuwa mgao unaongezeka kutokana na sababu zifuatazo:
i. Upungufu mkubwa wa maji katika mabwawa yetu ya kufua umeme hususani mabwawa ya Mtera, Kidatu, Hale, Kihansi na Nyumba ya Mungu. Uhaba huo umetokana na uhaba wa mvua katika vyanzo vya maji vinavyojaza mabwawa hayo hivyo kuathiri ufuaji umeme.
ii. Uhaba wa mafuta wa kuendeshea mitambo ya kufulia umeme ya IPTL na hivyo kusababisha upungufu wa ufuaji umeme kutoka Megawati 100 hadi Megawati 10 kwa sasa.
Ninachojiuliza, hivi Tanesco imeshindwaje kujua kuwa tatizo hilo linalojirudia mara kwa mara litatokea na kujihami nalo?
Pia najiuliza, hivi miaka kumi ijayo nchi hii itakuwa na huduma za umeme?
Halafu najiuliza hawa mainjinia waliojaa nchi hii wanafanya nini? Au kwa kuwasomesha, nchi hii ilicheza patapotea?
