Majeshi ya ulinzi ya Singapore yanaingia kwenye karne hii ya teknolojia kwa kishindo baada ya serikali ya nchi hiyo kuamua kuwapa askari wote wa nchi hiyo Ipads, imeelezwa na mtandao wa engadget.
iPads hizo ambazo ziko kwa mzabuni zikitengenezwa zitagawiwa kwa askari wa miguu, majini, na anga.
Askari hao watatumia iPads hizo kudownload muvi za kielimu kutoka katika mtandao wa jeshi.
Hata hivyo ukizingatia sheria za nchi hiyo inayomtaka kila mwanaume kutumikia jeshi kwa miaka miwili, Singapore itafurika kwa wingi wa iPads za bure.
