Wednesday, June 29, 2011

Google kuwalinda watumiaji wa gmail


Mtandao wa Google unabadilisha jinsi ya kuonyesha barua pepe zilizoingia kwenye anwani za watumiaji wake ili kuzuia barua pepe feki.
Habari hizo ambazo zimeletwa na mtandao wa softpedia zinasema kuwa kutokana na uwingi wa baruapepe feki mtandao huo umeamua kuwalinda watumiaji wake kwa kuwataarifu kama barua pepe zilizoingia ni halisi au feki.