Serikali ya China ambayo pamoja na wananchi wake ni watumiaji wazuri wa bidhaa za Linux, imeamua kuifanya Ubuntu kuwa Operating System ya kitaifa.
Wizara ya Viwanda na IT ya China kwa kushirikiana na wataalam wa nchi hiyo wa Kompyuta wako katika mchakato wa kuitengeneza Ubuntu iendane na kompyuta za nchi hiyo na kuipa jina la Ubuntu Kylin, (Sio yule mwanamziki wetu) hatua inayofikiriwa kuwa ni hatua ya nchi hiyo kuepuka makucha ya Marekani kwa kuzikwepa software za USA.