![]() |
| Christopher Robinson akiwa anagalagala kwenye fedha |
Kijana mwenye umri wa miaka 23 ambaye amekuwa akikwepa kulipa matunzo ya mtoto wake, ameponzwa na facebook baada ya kurusha picha akiwa anagalagala kwenye fedha
Akiwa amefaulu kukwepa kupeleka matunzo ya dola 150 (kama shilingi 240,00 za tanzania) kwa mwezi kwa miaka mitatu, alijikuta akitiwa mbaroni baada ya kutundika picha hiyo akiwa anagalagala kwenye fedha, picha ambayo gazeti la NY Daily News ikaichapisha na kusababisha vyombo vya dola vigundue kuwa aliwadanganya kuhusu kipato chake.
Christopher Robinson ameshtakiwa na inategemewa kuwa anweza kupewa kifungo kinachoweza kufikia miezi kumi na moja, alisema mwendesha mashtaka wa Milwaukee Prosecutor Kent Lovern.
