Thursday, March 28, 2013

JESHI LA MAJINI LA MISRI LAKAMATA WAZAMIAJI WAKIKATA WAYA ZA INTERNET ZINAZOKUJA TZ

Jeshi la majini la Misri limefanikiwa kuwakamata wazamiaji watatu wakitaka kukata nyaya za mawasiliano zinazokuja mpaka Tanzania.

Kukatika kwa waya za mawasiliano huko Misri imekuwa tatizo kwani kila zinapounganishwa hukatika tena. Haijulikani kama ni bahati mbaya au wazamiaji watatu ambao wamekamatwa na wanamaji wa Misri ndio wakataji wa nyaya hizo.

Baada ya tatizo la kukatika nyaya hizo wiki iliyopita kutatuliwa, utata umekuja baada ya kukamatwa watu hawa, kwani mwanzoni ilidhaniwa kuwa zimekatika kwa bahati mbaya lakini sasa watu wanajiuliza kama watu hawa hawahusiki na ukatikaji uliopita.
Tatizo lilianza wiki iliyopita wakati nyaya za SEA-ME-WE 4 (South East Asia–Middle East–Western Europe 4) zilipokatika jirani na Misri. Kampuni inayosimamia nyaya hizo ilijikuta kila ikitengeza hukatika tena, mpaka ikaamua kuwahamisha njia wateja wake ili waendelee kupata huduma kwani nyaya bado zimekatika.