Sunday, March 24, 2013

MUFTI MKUU AIPONDA TWITTER

Mufti Mkuu wa Saudia Sheikh Abdul-Aziz Al-Sheik
RIYADH, Saudi Arabia (AP) — Kiongozi mkubwa kabisa wa kidini wa Saudi Arabia ameuponda mtandao wa kijamii wa twitter kuwa ni baraza la wapenda mizaha.


Mufti Mkuu Sheikh Abdul-Aziz Al-Sheik, akiongea na viongozi wengine wa kidini wa Saudia Ijumaa hii, alisema kuwa mtandao huo ni ‘baraza la wapenda mizaha’ na ni sehemu ya taarifa zisizo sahihi na za upotoshaji.

Twitter imekuwa ikitumiwa na vijana wanaharakati kuleta upinzani nchini Saudia pia hata maofisa wa serikali wamekuwa wakitumia twitter kupeleka taarifa kwa wananchi.

Tamko hilo la Mufti limekuja siku moja na tamko la imam wa msikiti mkuu wa  Mecca lililosema kuwa ingawa watu wanahaki ya kujieleza, wawe waangalifu ili kujenga heshima na umoja wa kitaifa.