Tuesday, April 2, 2013

CURIOSITY YAHARIBIKA

Chombo Curiosity katika picha ya ilichojipiga chenyewe


Chombo kilichotumwa na shirika la uchunguzi wa anga za juu NASA katika sayari ya Mars,  kimeharibika kikiwa kazini katika sayari ya Mars.  

Chombo hicho Curiosity chenye ukubwa wa gari dogo, kinachojiendesha chenyewe kikiwa na maabara ya uchunguzi, kilichotua Mars August 6, 2012 kuchunguza hali ya hewa na geoloji ya sayari hiyo, kimepata hitilafu katika mfumo wake wa kumbukumbu na mpaka hivi sasa kinafanya kazi kutumia kompyuta zake za akiba wakati mafundi wake wakifanya bidii kurekebisha hali hiyo na wamefanikiwa kutengeneza kompyuta za chombo hicho na wanatarajia kupandisha data hivi karibuni.

Wataalamu hao wamepanga chombo hicho kianze kufanya kazi wiki ijayo ingawa sababu za hitilafu hiyo bado haijafaamika.