Baada ya kuufungia mtandao wa Pirate Bay, Uingereza imeanza
kuufungia mtandao maarufu kwa kudaunlodi wa Kickass torrents na mitandao
mingine ya torrents ambapo ghafla tu imeanza kuwa haipatikani au inachelewa
kupindukia kupandisha.
Kwa kawaida tovuti ikifungiwa mtumiaji ukijaribu kuifungua,
utapata meseji kukutaarifu kuwa mtandao huo umefungiwa, lakini kwa Torrents
maISP hawajajisumbua kutaarifu watumiaji.
Ingawa data hazionyeshi kama hatua hiyo inasaidia, pia
kufungia mitandao hiyo hakutaathiri watumiaji wa mitandao hiyo wanaopenda
kutumia bidhaa za bure kwani watahamia
mitandao mingine inayotengenezwa kila siku.