Idara ya polisi ya New York imeanza
kuwaelekeza maaskari na maofisa wa jeshi hilo matumizi mazuri ya Facebook na
mitandao mingine ya kijamii ili kulinda hadhi ya jeshi hilo.
Maelekezo hayo yalikuja kama amri ya
kuwataka waangalie wanachotundika kwenye mitandao na kuwahimiza wasiweke wazi
kuwa wao ni askari.
“Askari lazima aonyeshe uwezo wa
kufanya maamuzi na aonyeshe weredi wa kazi anapokuwa kazini.” Kilisema kimemo
hicho. Pia kilionya “Kurasa za mitandao ya kijamii inaweza kutumiwa dhidi yao
na kuharibu sifa ya Jeshi, kuingilia utendaji kazi, kuingilia upelelezi wa kesi
na kuathiri ajira za askari.”


