Thursday, April 4, 2013

SAMSUNG WABADILI STAILI YA MAUZO



Wakiwa hawajaridhishwa na magazilioni ya simu za Galaxy ambazo wameshauza, Samsung inaendeleza mapambano katika vita kubwa ya kibiashara inayoendelea kwa kuingia ubia wa mauzo na kampuni ya Best Buy Co., Inc.

Katika ubia huo Best Buy imekubali kuweka viduka vitakavyouza bidhaa za Samsung katika maduka ya 1400 ya Best Buy yaliyotawanyika sehemu mbalimbali duniani pamoja na maduka 900 yanayotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Best Buy Co., Inc ni kampuni ya kimataifa ya Marekani inayojiusisha na uuzaji wa bidhaa za kielektroniki yenye makao makuu Richfield, Minnesota, na ina matawi pamoja na Puerto Rico, Mexico, Canada and China.

Katika viduka hivyo vitakavyouza bidhaa za Samsung kama simu na vifaa vyake, Smart TVs na tablets, vitakuwa vikuhudumiwa na wahudumu walioajiliwa na Samsung ilil kumfanya mnunuzi  aone nini Samsung wanaweza kumpa kwa kiwango cha kumridhisha roho.

Sijui Apple na Microsoft watakopi na kupest staili hii ya Samsung?