Thursday, April 4, 2013

WALE WATU WA DATA





IBM imezindua teknolojia mpya ya kuchanganua data kwa upesi sana kuliko ilivyokuwa mwanzo kwa kutumia teknolojia ya Hadoop na kifaa cha PureData katika mkutano na waandishi wa habari  huko San Jose, Califonia, Jumatano iliyopita. Teknolojia hii itasababisha uchanganuaji wa data uwe wa kasi na zitachanganuliwa kwa kiwango kikubwa sana na kwa ufanisi mkubwa.
 
Kitu cha PureData cha IBM
Kwa malengo ya muda mrefu, IBM imepanga kuwasaidia wateja wake kuepuka tatizo la kugubikwa na mrundikano wa data za aina mbalimbali kwa kuwatafutia njia za kupambana mapambano yatakayoleta majibu mazuri zaidi na ufanisi utakaowapelekea kufanya kazi nzuri nyingi zaidi, alisema Bob Picciano, general manager wa information management ya IBM Software. “Ndio sababu vifaa vinatakiwa viwe na kasi na uwezo wa kufanya kazi kubwa sana na viwe rahisi kuvitumia.”