Dzhokhar Tsarnaev amefikishwa mahakamani kwa makosa ya kulipua mabomu mbio za
marathon za Boston, na akipatikana na
hatia anaweza kunyongwa.
Mwendesha mashtaka Eric Holder alitaja
makosa aliyoshtakiwa kijana huyo kuwa ni:
- Kosa moja la kula njama na kutumia
silaha za maangamizi dhidi ya binadamu na mali ndani ya Marekani na kusababisha
vifo.
- Kosa moja la kuharibu mali kwa kutumia milipuko ambayo ilisababisha vifo.
Kwa makosa hayo, iwapo atapatikana
na hatia anaweza kufungwa maisha au kunyongwa.
Mashtaka hayo alisomewa katika mahakama iliyohamia katika chumba cha hospitali anakolazwa kwa matibabu ya majeraha aliyoyapata wakati akipambana na polisi kabla ya kukamatwa.
