Friday, April 19, 2013
USIDATE DADA'KO
Katika jamii haikubaliki kabisa mtu kuanzisha uhusiano kimapenzi na ndugu wa karibu. Jamii nyingi zinachukulia jambo hilo kuwa ni laana kubwa kabisa wakati vitabu vya dini vinapinga jambo hilo kwa uzito mkubwa sana.
Tatizo linakuja; katika dunia hii ya leo ambayo watu tumetawanyika na thamani ya undugu imepungua sana na watu hawafuatiliani tena, utajuaje kama msichana unayemtamani si dada yako?
Maprograma nao hawajabaki nyuma katika kupambana na suala hilo, wao wametengeneza application ya smart simu ambayo inaweza kutambua sauti za watu na kujua kama ni za watu wenye.
Maprograma hao wa Iceland nchi yenye watu 320,000 tu ambayo kutokana na idadi ndogo ya wakazi, uwezekano wa kuingiliana ndugu umekuwa mkubwa sana, wamefaulu kutengeneza program inayoweza kutambua sauti kama zina uhusiano. Soft ware hiyo iliyotengenezwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Iceland imeelezewa ni muhimu; kwani hakuna kitu cha aibu kama ukigundua kuwa msichana uliyelala naye usiku kucha ni dada yako.
“Ni aibu sana unakwenda kwenye birthday ya mtoto wa babako mdogo, na kukuta kuwa ni msichana uliyemtosa hivi karibuni.” Alisema Einar Magnusson mtaalamu wa graphics wa Reykjavik.
Kauli mbiu ya software hiyo ni “Bump the app before you bump in bed,"
