Tuesday, April 16, 2013

BOMU LA BOSTON LILITENGENEZWA KWA MASUFURIA

Mabaki ya sufuria lililotumika kutengeneza bomu


FBI wamegundua kuwa bomu lililolipuka Boston, lilitengenezwa kwa vifaa rahisi kama misumari, nailoni, goroli, sufuria shinikizo na baruti, aina ya mabomu ambayo al qaida na wapiganaji wa Taliban pia wamewahi kuyatumia sana ingawa shambulio hili haliusishwi nao, alisema mFBI Rick DesLauriers ambapo vipande vya bomu hilo vilivyopatikana eneo la tukio vimekusanyawa na kupelekwa katika maabara ya FBI ambako wataalamu wataliunda tena ili liweze kusaidia upelelezi.

Siku za nyuma serikali ya Marekani iliwahi kuvitahadharisha vyombo vya usalama vyake kuwa masufuria na vifaa vya kutunzia vyakula vinaweza kutumika katika kutengeneza milipuko.