Monday, April 15, 2013

TORRENT ZAZIDI KUSHAMBULIWA



Ma ISP wa Italia wamezibloku tovuti 27 za BitTorrent zinazoruhusu watu wadaunlodi software za watu bila kulipia na wamedhamilia kuchukua hatua za kisheria za kimataifa kuzifuata tovuti hizo zinakotoka ili zichomolewe kabisa mtandaoni.

Baadhi ya tovuti hizo Rapidgator, BitShare, NowVideo, Uploaded, VideoPremium, NowDownload, QueenShare na  ClipsHouse.
Kufungiwa kwa tovuti hizo kunafuatia upelelezi wa polisi wanaochunguza makosa ya mtandaoni badala ya wenye makampuni ya software baada ya kampuni ndogo  ya kuuza cd kulalamika kuwa muvi yao ya katuni inatawanywa bure mtandaoni.