Mtu na mkewe wamekamatwa huko China kwa kutengeneza simu
feki za Apple.
Watu hao ambao hawajatajwa majina wamekuwa wakitengeneza
spea za bandi za simu za Apple kisha huzipeleka Apple na kudai wameletewa spea
mbovu, na Apple bila ajizi huwabadilishia na kuwapa spea halisi ambazo huenda
kuziunga na kupata simu orijino za apple.
Watu hao ambao wamekamatwa pamoja na wafanya kazi wao
watatu walikuwa wamekabidhi spea feki za Iphone 4s pea 121 ambavyo wangeviunga
na kupata Iphone mpya kabisa ambazo wangeziuza katika duka lao.
Wahalifu hao walishitukiwa na wafanyakazi wa Apple ambao
waliitaarifu polisi ambao hawakusita kuwatia mbaroni, wao na wafanyakazi wao.
