Friday, April 12, 2013

VIUNGO VYA BANDIA VYA WALEMAVU VYABORESHWA

Bosi wa Touch Bionics, Ian Steven
Kampuni ya Touch Bionics yenye makazi yake nchini Scotland, inayoongozwa na Ian Stevens imetangaza kuwa imefanikiwa kutengeneza mkono wa bandia wenye uwezo mkubwa zaidi kufanya shughuri za kilasiku za kibinadamu.




Viungo vya bandia ambavyo vinaunganishwa na mfumo wa neva uliobaki katika mlemavu, hutengenezwa kwa ushindani mkubwa na makampuni kama Otto Bock ya Ujerumani, RSL Steeper, Touch Bionics na mengineyo yamefanikiwa kutengeneza viungo vya hali ya juu sana kama vile vinavyoonekana katika sinema za science fiction ambapo kampuni ya Touch Basics ilianza biashara hiyo mwaka 2007 ambapo walitengeneza mkono waliouita i-LIMB Pulse na ukafuatiwa na I-Limb ultra.



Touch Bionics na washindani wake wamefanikiwa kuvifanya viungo hivyo kufanya kazi kwa kufuata hisia za binadamu.



Baadhi ya mambo yanayoweza kufanya na mkono huo yanaonyeshwa kwenye klipu hapo juu.