![]() |
| Chombo kinachotarajia kukamata kimondo kikiwa jirani na kimodo katika picha ya maelekezo ya mradi |
NASA wamezindua mpango kazi wa 2014 utakaogharimu $17.7 billion katika juhudi zao za utafiti wa anga za juu ambapo sasa hivi wanampango wa kukikamata kimondo (asteroid) na kukiweka jirani na mwezi ili wakifanye uchunguzi taratibu mradi unaotarajiwa kukamilika mwaka 2025.
Lengo la NASA ni kutuma chombo kinachojiendesha chenyewe kikakamate kimondo kimoja chenye uzito wa kilo mia tano na upana wa mita saba katika mradi uliofanyiwa uchunguzi na wanasayansi wa Caltech's Keck Institute for Space Studies huko Pasadena na kukileta jirani na dunia ili wanaanga wapate urahisi wa kukichunguza.
Ili kazi hiyo ikamilike kwa ufanisi, NASA wametenga $78 million kama kianzio cha mradi huo mkubwa utakaogharimu kitu kama $$2.6 billion mpaka utakapokamilika mwaka 2014.
