Nchi za wenzetu wameanza kuchukua hatua dhidi ya wezi wa smartphone wakiwa na malengo siku moja hata ukikabwa na vibaka, wasiitamani simu yako.
Mpaka hivi sasa hakuna njia ya uhakika ya kuzuia simu yako isiporwe na vibaka, lakini hivi sasa watengenezaji wa simu wameanza kuweka software zinazoonyesha simu ilipo mara itakapoibiwa. Kwa mfano; Apple wameweka Find My iPhone, software inayokuonyesha simu iliko, itapiga alarm, na ukitaka itaformat simu yako, Android wameweka software iitwayo Lookout ambayo itakuletea google map ikionyesha mahala ilipo, na itampiga picha mtu atakayejaribu kutoa password na kushindwa mara tatu na itakutumia kwa email picha hiyo.
![]() |
| Ramani utakayotumiwa na simu yako itakuwa kama hii |
Na hivi karibuni kampuni moja inayotengeneza software za kuloku laptop inayoitwa Absolute Software imependekeza kutengeneza software ya ulinzi ambayo haitafutika hata ikijaribu kuiflash simu yako na vifaa vyake vinawekwa katika simu mpya za Samsung galaxy zitakazotoka mwezi Mei. Akiielezea software hiyo CEO wa Absolute Mr. John Livingston, alisema kuwa software itamtaarifu mwenye simu iwampo kuna mtu anataka kuchezea simu hizo.
Itapendeza sana kama vibaka wamekukaba wakakuchukulia kila kitu wakakurudishia simu yako au ukipoteza simu, mtu aliyeiokota aipeleke polisi ili urudishiwe simu yako.

