WAMEFAULU KUUNDA FIGO
Watafiti kutoka katika hospitali kuu ya Massachusetts,
nchini marekani wamefaulu kuunda figo ya bandia ya panya ambayo imeweza kufanya
kazi vizuri inapopandwa kwenye panya.
Wataalamu hao walifanikiwa kutengeneza figo hiyo kwe kutumia figo za
binadamu na chembechembe za figo ya panya na ikafanikiwa kufanya kazi vizuri.
Hayo yameelezwa na Mtafiti wa Hospitali hiyo wakati akiongea na mtandao wa Nature
Medicine, Dr. Harald C. Ott
Akaongeza kuwa uwezekano wa kutengeneza kwa wingi fogo hizo kwa matumizi ya
binadamu utakuwa tayari hivi punde.