Pamoja na kuwa Windows 8
haijachanganya vya kutosha, Microsoft imeamua kuiondoa kati matumizi Windows XP
ambayo imedumu kwa miaka 11 na bado watu wanaendelea kuitumia, katika juhudi za
kuwafanya watu wahamie kwenye OS mpya.
Microsoft imefikia uamuzi huo ambapo itakapofika tarehe April 8, 2014, hakutakuwa na updates wala ulinzi kutoka Microsoft kwa
watumiaji wa XP hali itakayowafanya watumiaji wa XP kuhamia Windows 7 au 8 bila
kutaka.
Kutokana na takwimu za Net Applications mwezi wa 2013,
Windows XP, mpaka hivi sasa inatumiwa na asilimia 38 ya kompyuta zote duniani
na Microsoft watakuwa na wakati mgumu kuiondoa katika matumizi OS hiyo
inayopendwa sana duniani.
Wakiwa wamekatishwa tama na ufanisi wa Windows 8, watumiaji
wengi wameonyesha nia zao kuendelea kuitumia
XP pamoja na onyo la Microsoft kuwa watahatarisha data zao na kuzifanya
kompyuta zao kuwa wahanga wa mashabulizi ya hackers.
