Tuesday, April 9, 2013

TOVUTI YA KUIAGA XP

Katika kuuendeleza mpango wake wa kutoiendeleza XP, kampuni ya Microsoft imetoa tovuti itakayokuwa ikielekeza watu jinsi ya kuhama kutoka XP kwenda OS zingine na madhara ya kubaki XP baada ya tarehe April 8, 2014.
Cha ajabu Microsoft inatumia tovuti hiyohiyo kuipromoti Windows 8 pia, ikiwaalika watu kununua OS hiyo mpya kwa bei ya punguzo na Office 2013 pia ina bei punguzo mpaka mwezi wa June.
Microsoft wanaeleza kuwa kutumia XP baada ya  April, 2014 kutapelekea kuhatarisha usalama wa data za mtumiaji.