![]() |
| Voyager 1 |
Miaka therathini toka chombo cha utafiti wa anga za
juu Voyager 1, kinaweza kuwa kimefaulu kutoka nje ya mfumo jua wetu na kuwa
chombo cha kwanza kilichotengenezwa na binadamu kufanikiwa kutoka nje ya mfumo
jua, habari za kiutafiti zinasema.
Ingawa wanasayansi wanosimamia mradi huo wa Voyager
1 wanapinga taarifa hizo, gazeti la Geophysical Research Letters linakubaliana utafiti huo na kusema kuwa kuna
kia dallili chombo hicho kimeshatoka nje ya anga zetu.
Chombo hicho cha NASA kimekuwa kikielekea kwenye
kingo za Solar System, Aug. 25 kilituma taarifa za mabadiliko makubwa sana ya
miale na mionzi kikiwa zaidi ya maili bilioni 11 kutoka kwenye jua.
Wakati huohuo kilionyesha kuwa mionzi kutoka nje ya
solar system ikiwa imeongezeka kwa kiasi kikubwa kuliko wakati wowote toka
chombo kiondoke.
“Siku chache zilizopita mionzi ya heliospheric
imekuwa mikubwa sana na miale ya cosmic imezidi sana.” Alisema Bill Webber, falaki
waChuo kikuu cha New Mexico State nchini Marekani.


