Tuesday, April 23, 2013

MBUNGE ATAKA KAMPUNI ZA MAREKANI ZIFUKUZWE




Mbunge wa Kawe Halima Mdee ameitaka serikali kuangalia athari za mbegu zinazotoka nje kwani zina madhara makubwa na kampuni hizo zimepigwa marufuku kuingiza mbegu hizo katika nchi mbalimbali ikiwamo India, Argentina, Peru na Ufaransa.

Baadhi ya madhara ni pamoja na utahaira kwa watoto wanaozaliwa, utegemezi kwa kampuni hizo kwani lazima mkulima anunue mbegu kutoka kwao.

WAMEFAULU KUUNDA FIGO



Watafiti kutoka katika hospitali kuu ya Massachusetts, nchini marekani wamefaulu kuunda figo ya bandia ya panya ambayo imeweza kufanya kazi vizuri inapopandwa kwenye panya.

Wataalamu hao walifanikiwa kutengeneza figo hiyo kwe kutumia figo za binadamu na chembechembe za figo ya panya na ikafanikiwa kufanya kazi vizuri.

Hayo yameelezwa na Mtafiti wa Hospitali hiyo wakati akiongea na mtandao wa Nature Medicine, Dr. Harald C. Ott

Akaongeza kuwa uwezekano wa kutengeneza kwa wingi fogo hizo kwa matumizi ya binadamu utakuwa tayari hivi punde.

RAISI AKUTANA NA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA KIKRISTO




Viongozi wa dini wamewataka waumini kote nchini kulinda amani na umoja uliopo ili nchi isije ikaingia kwenye mgawanyiko wa kidini na kuleta machafuko hapa Tanzania.
Wito huo umetolewa na viongozi wa dini leo Ikulu ya Dar-Es-Salaam mara baada ya kikao cha pamoja baina ya viongozi wa dini na Rais Jakaya Kikwete.
Viongozi hao wa dini wamefika leo wakiongozwa na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Viongozi wengine wametokea Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) Seventh Day Advertist (SDA) na Baraza la Pentekoste Tanzania (PCT).
Mkutano huo umeanza kwa Askofu Ngalalekumtwa kusoma tamko lao la pamoja kwa Rais Kikwete ambalo ndilo limetoa muongozo wa mazungumzo hayo ya leo ambayo yamehusu Amani na Usalama wa Taifa na migogoro ya kidini ndani ya jamii.
Mkutano wa viongozi wa dini ya Kikristo Tanzania ni mojawapo ya jitihada za Rais Kikwete kutafuta muafaka na kutafuta utatuzi wa hali ya sintofahamu ambayo inanyemelea nchi yetu katika kipindi hiki.

PAMOJA NA UCHUMI KUPANDA, UMASIKI WAONGEZEKA TANZANIA

Ripoti ya hali ya uchumi duniani imeonesha kuwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliopindukia imeongezeka zaidi, huku jirani zetu wa Kenya na Uganda wakiwa wamepiga hatua zaidi katika kupunguza idadi ya watu wanaoishi katika umaskini wa kipato.
Kwa mujibu wa Ripoti ya World Bank iliyoripotiwa kwenye mtandao na Global Monitoring Report 2013, Watu wanaoishi katika umaskini wa kupindukia (wa kipato) ni 38.01% kwa Uganda, 43.37% kwa Kenya na Tanzania ni 67.87%.

Hata hivyo, kwa kuwa tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hivi karibuni Rwanda na Burundi wamejiunga nasi kwenye Jumuiya hiyo, tunaweza kujifariji kuwa sisi si wa mwisho Afrika Mashariki, kwani tunaizidi Burundi ambayo 81.32% wanaishi kwenye umaskini uliokithiri (wa kipato). Nchi nyingine ndogo, isiyo na bandari na iliyotoka kwenye matatizo ya mauaji ya kimbari na vita, Rwanda, ina asilimia ndogo zaidi ya maskini kulinganisha na Tanzania, ambapo 63.17% ya Wanyarwanda wanaishi katika hali ya umaskini.

ATHARI ZA UWEKEZAJI?

Mtoto huyu inasemekana anaishi katika moja ya vijiji vinavyozunguka migodi na inasemekana ameathirika na maji yanayomwagwa ovyo na migodi.

Monday, April 22, 2013

KIZIMBANI KWA KULIPUA MABOMU



Dzhokhar Tsarnaev amefikishwa mahakamani kwa makosa ya kulipua mabomu mbio za marathon za Boston,  na akipatikana na hatia anaweza kunyongwa.

Mwendesha mashtaka Eric Holder alitaja makosa aliyoshtakiwa kijana huyo kuwa ni:

  1. Kosa moja la kula njama na kutumia silaha za maangamizi dhidi ya binadamu na mali ndani ya Marekani na kusababisha vifo.
  2. Kosa moja la kuharibu mali kwa kutumia milipuko ambayo ilisababisha vifo.


Kwa makosa hayo, iwapo atapatikana na hatia anaweza kufungwa maisha au kunyongwa.


Mashtaka hayo alisomewa katika mahakama iliyohamia katika chumba cha hospitali anakolazwa kwa matibabu ya majeraha aliyoyapata wakati akipambana na polisi kabla ya kukamatwa.